FEMA Inaajiri watu katika Vermont

Release Date Release Number
018
Release Date:
Agosti 5, 2023

FEMA, kwa ushirikiano na Jimbo la Vermont, inaajiri wakazi wa jimbo hilo kusaidia na shughuli za marejesho baada ya mafuriko ya Julai, dhoruba kali, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya udongo.

Shirika lina nafasi kadhaa za kazi za muda mfupi, za wakati wote katika ofisi za muda za FEMA katika maeneo yaliyo karibu. Nafasi za muda ni za siku 120, lakini zinaweza kuongezwa kulingana na mahitaji ya janga. Nafasi zaidi zinaweza kufunguliwa ikiwa inahitajika.

Kufanya kazi na FEMA kutaruhusu wakaazi wa Vermont kuwasaidia majirani zao kurejelea hali kawaida. Kuajiri ndani ya jamii ni sehemu ya wajibu wa FEMA kuelekea jamii. Na kuajiri katika jamii kunasaidia kuimarisha wafanyakazi wa msaada wa majanga wa Marekani: wafanyakazi wengi wa sasa wa FEMA walianza kama waajiri wa jamii baada ya majanga makubwa katika majimbo yao.

Ili kujifunza zaidi na kutuma maombi, tumia kiunganishi hiki: USAJobs - Search. Au tembelea  USAJobs.gov, kisha tafuta “FEMA” chini ya “Keywords” na “Vermont” chini ya “Location.”

Viunganishi vya kazi vinavyopatikana kwa sasa viko hapa chini:

  • Mtaalamu wa Maeneo ya Mafuriko (Environmental Floodplain Specialist): USAJobs - Job Announcement – inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 8
  • Mtaalamu wa Uhifadhi wa Kihistoria (Historic Preservation Specialist): USAJobs - Job Announcement –inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 8
  • Mtaalamu wa Usafirishaji (Logistics Specialist): USAJobs - Job Announcement – inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 9.
  • Mtaalamu wa Ubunifu (Creative Specialist): USAJobs - Job Announcement – inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 9.
  • Mtaalamu wa Mahusiano ya Vyombo vya Habari (Media Relations Specialist): USAJobs - Job Announcement – inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 9.
  • Mtaalamu wa Mazingira (Environmental Specialist): USAJobs - Job Announcement – inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 10
  • Mtaalamu wa Kupunguza Hatari (Hazard Mitigation Specialist): USAJobs - Job Announcement –inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 10
  • Kiongozi wa Shuhuli za Wafanyakazi (Operations Task Force Leader): USAJobs - Job Announcement – inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 10
  • Mtaalamu wa Uhusiano wa Wakala wa Hiari (Voluntary Agency Liaison Specialist): USAJobs - Job Announcement – inafungwa saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.)  Agosti 10
  • Kila kazi itafungwa kufikia makataa au saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 p.m.) EST siku ambayo kikomo cha maombi kinafikiwa, chochote kitakachotangulia.

Nafasi fulani zinaweza kuhitaji kuendesha gari hadi maeneo yaliyoathiriwa. Ni lazima uwe raia wa Marekani, umri wa miaka 18 au zaidi, na uwe na diploma ya shule ya upili au GED ili kutuma ombi.

FEMA imejitolea kuajiri wafanyikazi waliohitimu ambao wanaonyesha unamnanamna ya taifa letu. Waombaji wote watazingatiwa bila kujali rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Serikali Kuu ni mwajiri wa Fursa Sawa.

Kupata habari mpya zaidi kuhusu urejesho katika Vermont, tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Region 1 katika Twitter twitter.com/FEMARegion1 au ukurasa wa Facebook ya FEMA facebook.com/FEMA.

Fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont kwenye Twitter kwa twitter.com/vemvt na kwenye Facebook katika facebook.com/VermontEmergencyManagement.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho