Kituo cha Msaada wa Majanga Chafunguliwa Plainfield

Release Date Release Number
014
Release Date:
Julai 31, 2023

WILLISTON, Vt. –Kituo cha Msaada wa Majanga (DRC) kitafunguliwa Plainfield mnamo Julai 31 kusaidia wakaazi wa Vermont walioathiriwa na mafuriko kurejelea hali kawaida. DRC ya pamoja, kituo cha muda kilichoanzishwa kwa ushirikiano kati ya Plainfield, jimbo la Vermont na FEMA, itasaidia waathirika kutuma maombi ya msaada wa FEMA, kupakia hati na kujibu maswali ana kwa ana.

Kituo cha Plainfield kinapatika:

Twinfield Union School
106 Nasmith Brook Road
Plainfield, VT 05667

Vituo tayari vimefunguliwa katika:

Waterbury Armory
294 Armory Drive
Waterbury, VT 05676

ASA Bloomer Building
88 Merchants Row, Suite 330
Rutland, VT 05701

Barre Auditorium
16 Auditorium Hill
Barre, VT 05641

Flood Brook School
91 VT-11
Londonderry, VT 05148

Zote zinafunguliwa siku 7 kwa wiki, saa mbili asubuhi (8:00 a.m) hadi saa moja jioni (7 p.m.)

Vituo vyote vinaweza kufikiwa na watu wenye ulemavu na mahitaji ya ufikiaji na utendaji, na vina vifaa vya teknolojia ya usaidizi. Ikiwa unahitaji makao ya kuridhisha au mkalimani wa lugha ya ishara, tafadhali piga simu kwa 1-833-285-7448 (bonyeza 2 kwa Kihispania). 

Wawakilishi kutoka Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani pia watakuwa katikati kueleza jinsi ya kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu ya SBA kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara na mashirika yasiyo ya kibiashara ya kibinafsi, na kutoa maelezo kuhusu kujenga upya ili kujenga nyumba zistahimili majanga zaidi.

Huhitaji kutembelea DRC ili kuomba usaidizi wa FEMA. Kutuma ombi bila kutembelea kituo, piga simu kwa nambari ya usaidizi ya FEMA kwa 800-621-3362, nenda mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au upakue FEMA App. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari ya huduma hiyo unapotuma ombi.

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa yeye ndiye mwathirika wa ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaozungumza lugha nyingi wanapatikana. 

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho