Msaada wa Kusafisha na Kutakasa Unapatikana kwa ajili ya Nyumba Zilizoharibiwa na Mafuriko

Release Date Release Number
13
Release Date:
Julai 30, 2023

Ikiwa nyumba yako iliharibiwa na mafuriko ya hivi majuzi ya Vermont lakini bado unaweza kuishi humo kwa usalama, FEMA inaweza kutoa hadi $300 ili kukusaidia kusafisha. Msaada huu wa Kusafisha na Kutakasa unakusudiwa kuwasaidia wamiliki wa nyumba na wapangaji kushughulikia haraka uchafuzi unaotokana na mafuriko ili kuzuia hasara zaidi na masuala ya usalama.

Unaweza kustahili kupokea msaada wa Kusafisha na Kutakasa ikiwa:

  • Unaishi katika kaunti ya Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham au Windsor.
  • Kulingana na ukaguzi wa FEMA, nyumba yako iliharibiwa na janga; au, ikiwa wewe ni mpangaji, maelezo ya ukaguzi ya hatua za kusafisha zinahitajika au tayari zimefanyika.
    • Ikiwa tayari umesafisha, hifadhi risiti zako za vifaa vyovyote, nyenzo au msaada uliyolipia.
  • Uharibifu haushughulikiwi na bima yako.
  • FEMA hubaini ikiwa makazi yako ya msingi yaliyoharibiwa na majanga ni salama kukaliwa.

Kwa ushauri kuhusu jambo la kufanya ikiwa nyumba yako ina kuvu, tembelea fema.gov/fact-sheet/mold-problems-and-solutions.

Ili kujiandikisha kupata msaada wa FEMA, tembelea DisasterAssistance.gov, pakua FEMA App au piga simu kwa 1-800-621-3362. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi. 

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaotumia lugha mbali mbali wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho