Ufadhili wa FEMA Hauchukuliwi kama Kipato kwa Hivyo Hautozwi Ushuru

Release Date Release Number
012
Release Date:
Oktoba 20, 2021

NEW YORK – Watu wanaopokea Malipo ya Uzeeni au msaada wowote wa serikali wasihofu kwamba Ufadhili wa mikasa wa FEMA huenda ukaathiri mafao yao.   

Ikiwa wewe ni mkazi wa kaunti za Bronx, Kings, Nassau, Queens, Richmond, Rockland, Suffolk au Westchester na ulituma maombi kwa FEMA ili kupata ufadhili wa mikasa wa kitaifa baada ya Kimbunga Ida, huna hatari ya kupoteza mafao mengine ya kitaifa ambayo ni haki yako.

Ufadhili wa mikasa wa FEMA hauchukuliwi kama mapato ya kutozwa ushuru.  Kukubali ufadhili wa FEMA hakutaathiri Malipo yako ya Uzeeni, Bima ya Taifa ya Afya (Medicare), Bima ya Taifa ya Afya kwa Watu wa Kipato cha Chini (Medicaid), Mpango wa Msaada wa Lishe ya Ziada (SNAP) au misaada ya programu nyingine za serikali.  

Ufadhili wa mikasa husaidia kulipia kodi ya makao ya muda, matengenezo muhimu ya nyumbani yaliyotokana na Kimbunga Ida, kununulia vitu vya kibnafsi na mahitaji mengine muhimu yanayohusiana na athari za mkasa ambayo hayasimamiwi na bima yako au vyanzo vingine vya ufadhili. 

Kuna njia mbalimbali za kutuma maombi ya ufadhili wa mikasa wa kitaifa:

  • Hostos College, 450 Grand Concourse, Bronx, NY 10451
  • Queens College, 152-45 Melbourne Ave., Queens, NY 11367
  • Medgar Evers College, 231 Crown St., Brooklyn, NY 11225
  • College of Staten Island, 2800 Victory Blvd., Staten Island, NY 10314
  • Michael J. Tully Park Physical Activity Center, 1801 Evergreen Ave., New Hyde Park, NY 11040
  • Rose Caracappa Senior Center, 739 NY-25A, Mount Sinai, NY 11766
  • Public Library, 136 Prospect Ave., Mamaroneck, NY 10543

 

Makataa ya kutuma maombi ya ufadhili wa mikasa wa FEMA ni Jumatatu, Disemba 6.

Kupata habari zaidi mtandaoni pamoja na vijitabu vya FEMA vinavyoweza kupakuliwa, tembelea DisasterAssistance.gov kisha ubofye “Information.”

Kwa rufaa kwenda kwa mashirika yanayosaidia katika mahitaji mahususi ya jamii, piga simu 211 au temebelea https://www.211nys.org/contact-us. Kwa wakazi wa mji wa York City, piga simu 311.

Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida, tembelea fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho